Saturday, April 20, 2013


WAREMBO WAGOMBEA KUMPA NAMBA MZUNGU...

Otilia Boniface kulia na Janeth Tingisha

Wanenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface na Janeth Tingisha mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa kali ya mwaka baada ya kutaka kutwangana makonde wakigombea kutoa namba zao za simu kwa buzi la Kizungu.

Tukio hilo lilitokea ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar ambapo awali Mzungu huyo alivutiwa na wadada hao hivyo kuwafuata na kuomba namba ya simu ya mmoja wao.

Kufuatia ombi la Mtasha huyo, kila mmoja alitaka apate nafasi hiyo ndipo wanenguaji hao waliposukumana na kufikia hatua ya Janeth kuchukua simu ya Otilia na kuipiga chini ila kwa busara za Mzungu huyo alichukua namba za wote.

DARASA LA SABA SASA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI

Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
 

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
 

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
 

Sifa zinazotakiwa
 
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
 

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:
 

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”
 

Vigezo
 
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
 

“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
 

chanzo:gazeti la mwananchi

Friday, April 19, 2013



MWANACHUO AVULIWA NGUO NA KUPEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUIBA VIATU

 Mrembo  huyu  aliyejitambulisha  kwa  ni mwanafunzi  wa chuo  kikuu  kimojawapo mjini Iringa akilia baada ya kupokea  kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara  eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya  kuiba viatu  vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa  akimpigia  simu mpenzi  wake  ili aweze kumkomboa baada ya  kutakiwa  kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .

----------------------------------------------------

Tukio la mrembo  huyo  kupokea  kichapo na kuvuliwa  nguo na  kupokonywa  simu yake na mikoba zaidi ya mitano  pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea  jumapili  wiki hii katika  eneo la Miyomboni mjini Iringa.

Akielezea juu ya mkasa  huo  wa aina yake  leo mfanyabiashara   huyo  mama Masawe  alisema kuwa eneo  hilo amekuwa na kawaida ya  kuibiwa  viatu katika  duka  lake la viatu  vya mtumba .....

Mama  huyu  anadai    kuwa  mbali ya  kukamatwa kwa mrembo  huyo  bado amepata  kukamata  vijana  zaidi ya  wawili watanashati ambao  wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na  kuishia  kuiba na kutoweka .

Binti   huyo ambaye  ni  mwanachuo   alifika  dukani hapo   na  kuanza kuchagua  viatu akijifanya  ni  mteja .....
 
Baada  ya  kuona  muuza  duka  ameangalia  pembeni, binti  huyo   alichukua  pea  mbili  za   viatu  na  kuzificha  kwapani  asijue  kwamba  pembeni  kulikuwa  na  mtu  mwingine  aliyekuwa  akimwangalia....
 
Alipoaga na  kutaka  kuondoka ndipo timbwili la  kichapo  lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba asipelekwe  polisi  na  asipewe  adhabu  kubwa  kwa  kuwa   ana ujauzito  wa miezi mitatu tumboni.

Alisema  kuwa  kutokana na maombi ya mrembo huyo  kupunguziwa adhabu  hakuweza kumfikisha  polisi  zaidi ya kumpa kichapo  cha kufa mtu na kumpokonya  mali  zote alizokuwa ametoka  kuiba katika maduka ya  Miyomboni mjini hapa pamoja na  simu  yake ya kiganjani .


Wednesday, April 17, 2013

Mwimbaji Bi Kidude aaga Dunia Zanzibar

 17 Aprili, 2013 - Saa 12:35 GMT
Mwimbaji nguli wa muziki wa tarabu nchini Tanzania Fatma binti Baraka, maarufu kama Bi Kidude amefariki Jumatano kisiwani Zanzibar akiwa na umri wa zaidi ya miaka 100.
Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mjukuu wake Fatuma Baraka ambaye pia ni muimbaji wa Taraabu. Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini kutokana na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.
Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.
Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa ikizorota kiasi cha serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani kuburudisha japokuwa alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi Februari mwaka huu.
Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake Zanzibar.
Wengi, hasa vijana wa kizazi kipya wanamfahamu Bi. Kidude kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba taarabu kwa kuchanganya lugha ya kiswahili na ile ya kiarabu. Nyimbo zake za kiarabu mara nyingi zimekuwa na ladha kama ile ya aliyekuwa mwimbaji gwiji wa Misri Ummu Kulthumu.
Sio uimbaji tu uliomfikisha Bi. Kidude alipofika, bali uwezo wake pia wa kutunga mashairi, kutumia ala za mziki kama vile kupiga ngoma na hata ngoma za unyago, vyote hivi vilimuweka Bi. Kidude katika nafasi tofauti katika jamii.
Alikuwa na tabia ya kumwita kila mtu 'mwanangu,' ingawa yeye mwenyewe hakubahatika kupata mtoto. Katika mahojiano aliyofanyiwa na vyombo mbali mbali vya habari, mwenyewe alisikika akisema, ingawa alikuwa na hamu ya kupata mtoto, lakini Mwenyezi Mungu hakumjaalia.
Katika miaka ya hivi karibuni, Bi. Kidude alishirikishwa sana na wasanii wengine katika kazi zao. Miongoni mwao ni Ahmada Amelewa, Fid Q Juhudi za Wasiojiweza.
Mbali na hayo, mashirika mbali mbali yakiwemo ya kibiashara na yale yasiyo ya kiserikali yaliona mvuto aliokuwa nao Bi. Kidude katika jamii, hivyo wakamtumia katika matangazo mbali mbali maarufu likiwa lile la kutokemeza Malaria.
Ni bibi aliyebahatika kusafiri takriban duniani kote, na vilevile katika maisha yake alijinyakulia tuzo lukuki. Miongoni mwa hizo ni ile ya 2005 WOMEX ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki.
Katika siku zake za mwisho, Bi. Kidude alikuwa akiumwa, lakini wengi wanahusisha kuumwa kwake na utu uzima aliokuwa nao.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa wote, lakini zaidi ni wanamziki wa kizazi kipya waliokuwa wakimuona Bi. Kidude ni nyanya yao.